Kwa mujibu wa kitengo cha kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, Chama cha Vatan cha Uturuki kilifanya mkutano mjini Bursa kwa anuani isemayo “Matokeo ya muqawama wa Iran katika mchakato wa Asia inayoibuka”. Katika mkutano huo, Doğu Perinçek, rais wa Chama cha Vatan, Ali Özgündüz, mwakilishi wa muhula wa ishirini na nne wa Bunge la Istanbul, pamoja na Abolqasem Tahmasebi, mwanadiplomasia mwandamizi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, walihutubia, Programu hiyo ilipokelewa kwa hamasa kubwa na washiriki, na waliohudhuria waliwauliza wazungumzaji maswali mengi, Inafaa kutajwa kwamba mkutano huo ulidumu kwa takriban masaa matatu.
Programu hii ilianza kwa dakika moja ya kimya na kusomwa wimbo wa taifa wa Uturuki, Dilek Çınar, mkuu wa tawi la jimbo la Bursa la Chama cha Vatan, katika hotuba yake ya ufunguzi alisema kuwa; lengo la mkusanyiko huo ni kuchunguza “ushindi wa Iran” na nafasi ya Uturuki katika mabadiliko mapya ya kikanda, akisema kwamba Iran “imewapigisha magoti” Marekani na Israel, alieleza: “Marekani haikufikia hata moja ya malengo yake ya kisiasa, walishindwa nchini Iran na jambo hili pia lina mafunzo muhimu kwa nchi yetu.”
Jiografia ya mashujaa
Doğu Perinçek katika hotuba yake huku akirejelea kuundwa kwa mfumo mpya wa dunia alisema: “Dunia mpya iko katika hatua ya kuanzishwa, na katika mstari wa mbele wa dunia hii mpya kuna kambi ya ubinadamu, Iran inapigania ubinadamu na pia inaipigania Uturuki, Palestina, Hamas, Hizbullah na Yemen pia wanapigania wanadamu wote, Asia Magharibi sasa imegeuka kuwa jiografia ya mashujaa.”
Pia aliitaja Uturuki kuwa nchi iliyopo mstari wa mbele wa mabadiliko ya kikanda na kudai kuwa; Marekani Israel na Ugiriki zimeunda muungano dhidi ya Uturuki katika mashariki ya Bahari ya Mediterranean, Perinçek akirejelea mazoezi ya pamoja ya kijeshi ya nchi hizo alisema: “Mazoezi ya kuvuka mto Meriç yana maana ya maandalizi ya kuingia katika ardhi ya Uturuki, bado mizinga na vifaru vya Marekani na Israel haijafika kwenye milango ya nyumba zetu, lakini maandalizi haya ya kijeshi yanatuonya kuhusu siku zijazo.”
Hatuwezi kutazama kutoka barazani
Rais wa Chama cha Vatan alisisitiza: Uturuki haiwezi “kutazama kutoka barazani” vita vya Wapalestina huko Ghaza, muqawama wa Yemen na mapambano ya Hizbullah ya Lebanon, na akaongeza: “Ikiwa leo midomo ya bunduki imeelekezwa upande wa Uturuki, basi kesho risasi zake pia zitafyatuliwa kuelekea kwetu.”
Hesabu za muqawama
Perinçek aliutaja muqawama wa Iran kuwa matokeo ya “kutafuta shahada, busara na elimu”, na akasema kwamba; Iran kwa kupanga mkakati sahihi imeweza kusimama dhidi ya mashambulizi ya Marekani na Israel, alisema: “Pembeni mwa Iran, kambi ya kibinadamu imeundwa; kuanzia Urusi na China hadi nchi za Kiarabu, Nicaragua, Cuba, Mexico na hata Wakristo wa Ulaya, waziri Mkuu Mkatoliki wa Hispania pia yupo katika kambi hii, Iran imeweza kuunda mazingira ya kimkakati, ambayo sisi pia tunapaswa kuyajifunza vizuri.”
Aliongeza: “Iran imemuelewa vizuri adui yake ni nani na rafiki yake ni nani, hii ni hesabu ya kisiasa, na Uturuki pia ili kujizuia dhidi ya vitisho vya Marekani na Israel inapaswa kuunda mlingano kama huo.”
Marekani na Israel zinaogopa mlingano huu
Perinçek alisema wazo la muungano wa “Uturuki, Urusi, China na Iran” kwa miaka mingi lilikuwa likitolewa na Chama cha Vatan, lakini sasa mtazamo huo unaendelea kuimarika ndani ya muundo wa serikali ya Uturuki pia.
Alisisitiza: “Marekani na Israel zinaogopa mlingano huu, kama alivyosema pia Bw. Devlet Bahçeli, mbele ya muungano wa uovu wa Marekani na Israel, lazima uundwe muungano wa kibinadamu wa Uturuki, Urusi, China na Iran.”
Mipango mitatu kwa ajili ya mustakabali wa Uturuki
Rais wa Chama cha Vatan cha Uturuki kisha alielezea mihimili mitatu mikuu ya mpango wake wa kisiasa na kusema kwamba: Uturuki Inapaswa kuelekea katika uchumi unaozingatia uzalishaji na kurudisha nchini mtaji uliokusanywa katika benki za Magharibi, alidai kuwa takriban dola bilioni 500 mali za matajiri wa Kituruki zimehifadhiwa katika benki za London, New York na Uswisi, na serikali inapaswa kwa mamlaka ya kisheria kuzirudisha fedha hizi katika mzunguko wa uzalishaji wa ndani.
Perinçek akirejelea mshikamano wa kitaifa nchini Uturuki alisema: “Marekani na Israel walijaribu kuigawa Uturuki, lakini sasa hata Wakurdi wetu wameingia katika mchakato wa ‘Uturuki isiyo na ugaidi’ au kwa maana sahihi zaidi ‘Uturuki iliyoungana’. Tutaiunganisha Uturuki katika serikali na taifa.”
Aliendelea kwa kutaka kuundwa kwa “Uturuki ya watu wenye heshima” na alisema: “Tunaitaka Uturuki ambayo watu wanaishi kwa kazi na juhudi, si Uturuki ya waporaji na ufisadi, utamaduni wa ubinafsi na kujipendelea umeingia katika jamii yetu kutoka Magharibi, na tunapaswa kuhuisha tena utamaduni wa kujitolea na maadili ya kiroho.”
Muungano na Iran, Urusi na China si uchaguzi rahisi
Perinçek katika sehemu nyingine ya hotuba yake alisisitiza kuwa: “Muungano huu si tu chaguo la sera za kigeni; bali ni njia ya kuijenga Uturuki mpya; Uturuki inayojengwa juu ya undugu, uzalishaji, mshikamano na maadili ya kiroho.”
Maoni yako